Tangu utotoni, nikiwa mshabiki mkubwa wa mpira wa Tanzania, haswa Simba ambako Baba yangu alikuwa Mweka Hazina enzi za akina Mwemeja, nilikuwa na hakikisha na enda uwanjani ku angalia kandanda na kuisapoti timu yangu. Nilikuwa mtu mwenye bahati nzuri ya kuwa moja wao ku enda kambini ku kaa na wachezaji, ku ongea nao na wengine tuki kaa nyumbani kula pamoja. Hadi leo, ambako nimefikia umri wa miaka 21, na ji ulizaga swali moja: "Je, Tanzania kweli tuna mpira?"
Ni swali ambacho kina maoni tofauti kati ya watu, lakini ni dhahiri kabisa kusema kuwa, Tanzania, tumeuacha mpira nyuma na ku elekeza uzembe, hela na siasa kuiharibu mpira wetu.
Katika makala hili, nitaizungumzia sera 5 kati za nyingi zilizopo, ambazo zimesababisha kifo cha mpira wa Tanzania, na kuiweka iwe Simba na Yanga tu!
Uongozi:
Ukitulinganisha na nchi tofauti katika Bara la Afrika, sie tuna wachezaji wenye kipaji na uwezo mkubwa, ila ni uongozi wa vilabu ambazo zina sababisha kifo cha soka la Tanzania. Kutoka enzi za wachezaji kama Akilimali, Machinga, Ally Mayai, na leo Kipre Tchetche, Ngassa, hakuna uongozi hata moja walichokifanya kitu chochote ku sababisha maendeleo ya mpira wetu.
Kila aliekuja madarakani, ame ingiza hela, aka sajili wachezaji aliewapenda, aka leta kocha anaemsifu na mwishoni aka shinda ligi katika mwaka wake wa kwanza madarakani, mwake uliofuata, timu pinzani ikampindua Mwenyekiti, nae aka fanya alicho fanya mpinzani wake, na sakata hili lika endelea hadi leo.
Hakuna kiongozi ata moja aliekuja madarakani na kufanya walichofanya Azam Fc, bali wote waka elekeza nguvu zao za kuwa wale ambao wata shangiliwa na mashabiki waki ingia uwanjani!
Hakuna kitu kama hilo katika mpira, ata mmiliki wa TP Mazembe hakufukuza makocha kama tulivyofanya sie katika vilabu vyetu, bali, aka elekeza nguvu zake kuiboresha vifaa vya klabu na mwishoni, aka kuta mafanikio yaliopo leo na zina onekana dhahiri kabisa.
Kuna siku nili enda uwanjani ku angalia mechi kati ya timu mbili kongwe za Tanzania, na nika fanikiwa kuwa na baadhi ya "wazee wakubwa" wa klabu mmoja kati ya hizo mbili, na ghafla mmoja wao aka soma kikosi kitakacho cheza, na mwishoni kusema, leo mwalimu ka taja kile tulichomwandikia! Ni pale nika kaa, na ku ji uliza, "je huyu aliopo kwenye kiti cha benchi la ufundi, ni kocha au ni mtumishi ambaye ana fuata ana cho ambiwa na ma bossi wake?
Je ni wapi umeona kwamba Mwenyekiti wa timu fulani anampangia kikosi kocha? Na ni viongozi hawo ambao hawa cheleweshi kumfukuza kocha kwa kusema "hatujafurahishwa na matokeo." Itakuwaje umfurahishwe na matokeo wakati nyie ndio mnao panga timu?
Ki binafsi, kila siku nawa ambiaga marafiki na wadau wa soka, kwamba kama kuna timu ambayo ita fanikiwa kufanya vizuri ni Azam Fc, lakini, ghafla nae waka anza kufuata nyanzo za wapinzani na kumfukuza kocha wao. Na haikuchukua miezi kadhaa, kabla kumrudisha kazini na uongozi huo huo waliemfukuza!
Viongozi wa vilabu ya Ligi Kuu Tanzania, pamoja na viongozi wa TFF, wanatakiwa wachunguze maamuzi
zao kabla za kuzitangaza katika vyombo vya habari, na baadaye kusikitika.
Mara nyingi uamuzi wa kijinga unaofanyiwa na hao viongozi, unaiathiri timu kwa njia tofauti, na kusababisha kiwango cha mpira kushuka. Kuwa fungia wachezaji kwa utovu wa nidhamu, kuihujumu timu, kutoelewana na mwalimu na viongozi, haya ni mifano ya maamuzi yanayofikiwa na viongozi wa vilabu vyetu. Waki ulizwa kuwasilisha ushahidi, wana beza kwa kusema, hayo ni masuala ya klabu na hatuweki hadharani!
Ninakumbuka, niki enda ku angalia mechi fulani na nika fanikiwa ku ingia ku keti chumba cha kubadilisha
nguo na wachezaji, ghafla nika ona mchezaji mmoja wa kigeni aka ambiwa leo huta anza kwasbabu tuna shaka kwamaba utaihujumu timu. Kuna habari zime tu fikia kwamba umepokea kiasi fulani cha fedha na utaihujumu timu, kwa vile uta anzia benchi. Na hayo maneno ni dakika chache kabla ya mchezo ku anza, je fikiria hali ya Kocha wakati huo. Je ni nini kitakacho kichwani mwake, ata badilishaje formeshen ya timu, na hakuna ata kiongozi mmoja aliewasilisha malalimiko kwa mwalimu, badala yake, waka chukua uamuzi mikononi mwao. Na si kitu cha ajabu, kwamba ni mchezaji huyo huyo ambaye alipotoka benchi na ku cheza, aka sababisha magoli mawili kilichoipa ushindi timu yake.
Tatizo la uongozi kushindwa kufanya kazi kwa utaalamu ambacho kina sababisha matatizo kadhaa. Mfano mmoja ambao ni tatizo kubwa sana, ni jinsi viongozi wanaishughulikia swala la uhamisho wa wachezaji na mikataba yao. Swala hilo nitali fafanua zaidi katika article lifuatayo, ambacho kita tolewa wiki ijayo.
Pamoja tujenge, na kuendeleza mpira wa Tanzania!
No comments:
Post a Comment